Baada ya Mwanza Mwanza na August 13, Majani na Fid Q waingia jikoni tena
Pamoja na Huyu na Yule iliyofanywa na Master Jay kumtambulisha vema Fid, ni P-Funk Majani ndiye anapewa credits nyingi zaidi za kumweka kwenye chart rapper huyo kutoka Mwanza ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda. Majani kupitia Bongo Records, ameshafanya hits kadhaa za Fid zikiwemo Mwanza Mwanza, August 13 na Chagua Moja.
Na sasa jamaa hawa wawili wameungana tena ambapo Majani kama kawaida yake amesimimia mdundo na masuala ya upishi zaidi na Fid kuspit rhymes zenye sumu kwenye mdundo wa Kinywele Kimoja.
Ngoma hiyo itakuwa ya tatu kutoka kwenye albam yake Kitaalojia baada ya Fid kutweet, “KitaaOLOJIA ‘ The completion of the trilogy ‘ 1-#ieLeweMitaa √ 2- #SihitajiMarafiki √ *next release lini? P_Majani anajua #Tuombeane Dua na Majani kujibu, “it’s my first song to mix this week, Video ASAP!!!! I can’t stop replaying that trak.”
Tunaisuburi kwa hamu.
No comments:
Post a Comment